Unknown Unknown Author
Title: ALICHOKISEMA JPM JANA BAADA YA KUPEWA KOFIA YAKE CCM
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa CCM Ndugu, John Pombe Magufuli: Katika uongozi wangu, mtu atakayetumia rushwa hatachaguliwa au  hatateuliwa kugombea nafasi...
Mwenyekiti wa CCM Ndugu, John Pombe Magufuli: Katika uongozi wangu, mtu atakayetumia rushwa hatachaguliwa au  hatateuliwa kugombea nafasi yoyote.

Hatuhitaji wana CCM maslahi, au wana CCM ambao wapo CCM kwa kuwa wanamuabudu mtu fulani.

Nataka CCM inayofanya kazi siyo CCM ombaomba, nata CCM inayojitegemea na siyo CCM inayotegemea wafadhili.

Katika miezi 8 tumefanya mengi ikiwemo kuondoa wafanyakazi hewa, na kama CCM kuna wafanyakazi hewa wataondoka.

Ng'ombe akikatika mkia humzuii kuingia kwenye zizi, lakini akifika kwenye zizi, wengine watajua kuwa huyo hana mkia.

Watanzania wanahitaji maendeleo, maendeleo kwanza, siasa baadaye, nawashukuru sana wanasiasa wa upinzani mliofika.

Nimeamua sherehe za mashujaa za mwaka huu kitaifa zifanyike Dodoma. Baba wa Taifa alipoamua kuhusu Dodoma hakutania.

Kabla sijamaliza kipindi changu cha miaka mitano nitahakikisha serikali nzima imehamia Dodoma.

Kama wabunge wote wakati wa bunge wanakaa Dodoma, wajumbe wote mmekuja Dodoma, sioni sababu ya mimi kubaki Dar Es Salaam.

Siku nitakayohama Dar Es Salaam naamini Makamu wa Rais pia atanifuata, na mawaziri wote watanifuata.

Abdulrahman Kinana amewasilisha rasmi barua ya kujiuzulu ambayo imesomwa na Mwenyekiti Dk. Magufuli na Baada ya kupokea barua, nimeamua bila kumuuliza mtu, kwamba Kinana na sekretariet yote waendelee.

Nataka Kinana na wenzake wakasimamie utekelezaji wa haya yote niliyoyaagiza katika chama.

JE KWA HATUA HIZO ANAZO ZICHUKUA JPM, UPINZANI UTAKUFA?

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top