Miaka kadhaa iliyopita Kijana mmoja alikutana na msichana katika moja ya mitandao ya kijamii. Yule msichana hakuwahi kuwa na picha ya yule kijana. Ila kijana alikuwa nayo moja ya yule msichana aliyoitoa kutoka kwenye profile.
Walianza ku chat kwa Email kila siku na wakawa marafiki wakubwa sana na walioelewana.
Baada ya miezi michache, walianza kupendana na wakawa wapenzi. Ni mpaka wiki chache baadae yule msichana alikatisha mawasiliano ghafla.
Meseji za yule kijana zilikuwa hazijibiwi wala kuonesha kwamba zimepokelewa.
Kijana alisubiri muda mrefu sana lakini hakupata kujibiwa. Wiki zilisonga, kijana akiendelea kusubiri lakini hakupata mrejesho wowote wenye manufaa.
Kijana alimpenda sana yule msichana.
Aliumia sana na akaingiwa na hofu huenda kuna jambo baya limemtokea mpenzi wake, hakupata raha hata kidogo na hakua na namna ya kuweza kumfikia.
Baada ya miezi michache kijana alikubaliana na hali halisi kwamba mahusiano yao yamekwisha.
Aliumizwa vibaya sana moyoni.
Kila siku alikuwa akisoma meseji ambazo walikuwa wakichati, mipango waliyokuwa wakipanga pamoja na mengineyo.
Baada ya miaka kadhaa, kijana alianza masomo ya chuo kikuu kujiendeleza kielimu. Alikaa mbali na wanawake kwakuhofia kupenda tena na kuumizwa.
Ila baadae kidogo msichana mmoja pale chuoni alimteka kiakili, yule msichana alikuwa mzuri kweli.
Kwake aliona itakua ngumu kumkabiri yule msichana kwa vile hajazungumza na msichana yoyote tokea ajiunge na kile chuo.
Ila kulikuwa na kitu cha kipekee kilichomvutia yule kijana kwa yule msichana. Ni kama alimfananisha na mtu fulani, isipokua huyu alikuwa na kovu kubwa upande wa kulia wa uso wake na kwenye paji la uso.
Hivyo kwa ujasiri alimfuata na kumueleza kuwa amekua akimpenda tokea mara ya kwanza amemuona katika viunga vya chuo, ila yule msichana alimkataa kata kata.
Mvulana: Samahani, kama nitakuwa nimekukosea heshima kwa kukwambia kwamba nimekupenda.
Msichana: Usijali, sio kosa lako....ni kwamba tayari niko kwenye mahusiano na mtu.
Mvulana: oh okey, samahani sana! Kumbe ushawahiwa.
Msichana: Naweza nikasema hivyo, nilimpenda kijana mmoja miaka kadhaa iliyopita alikuwa akiishi mji huu huu, ila kutokana na hali ambayo haikuweza kuzuilika tulipotezana.
Ila sasa nipo hapa kwa ajili ya kusoma na pia kumtafuta kama nitamuona, maana aliniambia hiki ndio chuo cha ndoto yake.
MVULANA: Wow! Hata mimi nipo kwenye hali kama yako, tulipotezana na msichana wangu bila sababu ya msingi.
MSICHANA: Kweli? Jina lake anaitwa nani?
MVULANA: Anaitwa Alisha. Alisha Mikidadi.
Yule msichana alimkumbatia kwa nguvu yule kijana huku machozi yakimtiririka. Alilia na kumwambia yule kijana mimi ndio Alisha!
Mvulana: Kwanini uliniacha kwenye kiza kinene na vile me nilikuwa nimeshakupenda Alisha?
MSICHANA: Mara ya mwisho nilikwambia tunaenda kwenye harusi, tulipata ajali ya gari na nikalazwa hospitali mwaka mzima nikiwa nimepooza upande mmoja.
Sikuwa naweza kuongea wala kufanya lolote. Kila mtu alidhani nitakufa. Ila nashukuru Mungu kiu yangu ya kukuona iliniweka hai.
Nimepona kama miezi sita hivi iliyopita. Nimepona ni mzima kabisa.
Na nilivyopata nafuu, nilipanga nije hapa, nakumbuka uliniambia hiki ndio chuo utakachokuja kusoma mwaka huu.
Hivyo namimi nika apply hapa hapa. Ila nilikuwa na hofu utakua ushapata mwanamke mwingine
MVULANA: Pole sana Alisha kwa yaliyokupata, Alichokiweka Mungu kwa ajili yangu, kitakua cha kwangu.
Nashukuru Mungu tumekutana tena pamoja. Nakupenda sana Alisha.
Wapenzi hawa walifunga ndoa baada ya kumaliza masomo yao.
Hivi sasa Wanaishi kwa amani na furaha na Mungu amewabariki na watoto watatu.
Leo nami nakuombea kwa Mungu kile kilichopangwa kuwa chako siku zote kikawe chako. Chako peke yako. Kuwa na matumaini na Mungu wako, nae atakufanyia yale yaliyo mema kwako, AMEN!
Share na marafiki zako
Post a Comment