Klabu ya Simba kwa furaha iliyochanganika na huzuni kubwa,kesho inatarajiwa kumuaga LEGENDARY wake Mussa Hassan 'Mgosi' kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Timu ya URA ya nchini Uganda,
Mchezo utakaonza saa kumi alasiri katika uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es salaam
Mgosi aliyeitumikia klabu yetu kwa mafanikio na nidhamu kubwa ameamua kustaafu kucheza soka ya ushindani na kuwaachia vijana,ataagwa kwa heshima zote kama mchezaji aliyeacha alama kubwa 'LEGACY' kwenye klabu yetu.
Kwa nidhamu aliyoionyesha na mapenzi yake kwa klabu. Simba imeamua kuendelea kumtumia kama meneja wa timu kuanzia kesho,mara baada ya kustaafu rasmi.
Huku Abbas Alli akiwa mratibu wa timu atakaeshirikiana na Mgosi kwenye usimamizi wa masuala ya timu kwa ujumla.
Nitumie fursa hii kuwaomba sana wana Simba tujitokeze kwa wingi kwenye mchezo huo muhimu na maalum ili muweze kuona kikosi chenu kwa mara ya mwisho,kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya Vodacom mwishoni mwa wiki ijayo.
Kwa sasa timu ipo kambini na kocha wetu Joseph Omog ameahidi kushusha 'mashine' zake ili sio tu kuwafunga URA bali pia kuonyesha soka safi itakayoburudisha kama ilivyo falsafa ya kudumu ya timu ya Simba.
Halikadhalika klabu inawashukuru klabu ya Azam ambao tumeshirikiana nao kuileta timu hii ya Uganda ambayo imeonyesha uwezo mkubwa kwenye mechi yao dhidi ya vijana kutoka Chamanzi.
Niwaarifu pia kesho kutakuwa na udhibiti mkubwa wa uingiaji mpirani, sambamba na udhibiti wa walanguzi wa tiketi ambazo zitauzwa kwa kiingilio cha Shilingi 20,000 kwa VIP A.Elfu 15,000 kwa VIP B na C, na shilingi 5,000 kwa mzunguko.
Mwisho niwajulishe ulinzi na usalama kwenye mchezo huo utakuwa ni kiwango cha juu..walanguzi na wauzaji tiketi feki wajihadhari..hakutakuwa na msalie Mtume kesho.klabu haitajali cheo wala umaarufu wa mtu.
Matarajio yetu kila mtu atajidhibiti mwenyewe kuhakikisha mapato halali yanapatikana na usalama unakuwa wa kutosha ndani na nje ya uwanja.
Nb. Tumejitahidi kuweka muda mzuri zaidi ili kuwawezesha watazamaji wawahi mechi za ligi kuu ya Uingereza zinazotarajiwa kuchezwa kesho.
Imetolewa na
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI
SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA
About Author
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Advertisement
Related Posts
- NDUGAI ATIA MGUU OPERESHENI UKUTA, WENYEWE WAMPA MASHARTI HAYA: BOFYA HAPA KUPATA KILICHOJIRI15 Aug 20160
TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU MAWASILIANO ifastar1991@gmail.com Read more »
- MAVUGO; MTAOMBA PO TU....!!! AWACHAMBUA YONDANI, BOSSOU, ACHEKA FIGISU ZAISHA13 Aug 20160
TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU MAWASILIANO ifastar1991@gmail.com Read more »
- KUTANA NA PROF. ROGO ROBERT KIMARO WA HUKO UoC13 Aug 20160
Taarifa zinazo zagaa katika mitandao ya kijamii zinasema huyu ni Prof. Rogo Robert Kimaro: Bingwa...Read more »
- Weeeenh....!!!! Zari Hapimiki, Si kipesa Tu hii Sasa awashika wachonga "ngenga" Waliomwambia Anategemea Pesa Za Diamond13 Aug 20160
Mama Tiffah akiwa kwenye Moja ya swiming pool ya nyumba hiyo Kupitia ukurasa wa Instagram Wa ma...Read more »
- SIRI ZAVUJA KUMBE.....DIAMOND KUMVISHA HARMONIZE "DERA" KATIKA NGOMA HII....!!!!13 Aug 20160
Kutoka katika ukurasa wa facebook wa msanii Harmonize, amesema ......Mhhh copy! copy! copy!..... ...Read more »
- ACHANA NA ZILE ZINGINE; UNAAMBIWA HIZI NDIZO KATUNI 4 ZILIZOPATA UMAARUFU KATIKA MITANDAO YA KIJAMII: BOFYA HAPA KUZICHEKI13 Aug 20160
USISAHAU KU-LIKE NA KU-SHARE PAGE YETU YA "UMBEA ONLINE" KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.