Unknown Unknown Author
Title: SENDEKA AWABANA MAFISADI, AWAKOMALIA MAHAKAMANI NI LAZIMA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Chama cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuwafikisha mahakamani  mafisadi na  watumishi wote wa umma waliofukuzwa kazi kwa sababu mbalimbal...
Chama cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuwafikisha mahakamani  mafisadi na  watumishi wote wa umma waliofukuzwa kazi kwa sababu mbalimbali, ikiwamo kuisababishia hasara  kutokana na watumishi hewa.

Msemaji chama hicho, Christopher Ole Sendeka amesema hayo alipokuwa akizungumza katika sherehe na misa ya shukrani ya Diwani wa Kata ya Gilai, Bomba Simon Oitesoi aliyepita bila kupingwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Sendeka amesema wananchi wanamuunga mkono Rais John Magufuli katika jitihada zake za kurejesha nidhamu na uwajibikaji serikalini kwa manufaa ya umma.

Amesema kwa kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Magufuli katika kazi mbalimbali alizozifanya zimejenga imani kubwa ya wananchi kwa chama hicho na sasa hatua ya kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote bila kujali nafasi zao inasubiriwa na wengi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top