Unknown Unknown Author
Title: JPM AWAFUNGA MIDOMO, MWENYEWE ACHEKA TU KWA KINACHOENDELEA MITANDAONI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Leo mchana Rais JPM alikuwa anaongea na Wakurugenzi wa Wilaya,Miji na Majiji Ikulu Dsm Moja ya jambo alilolisema limemsikitisha ni mita...
Leo mchana Rais JPM alikuwa anaongea na Wakurugenzi wa Wilaya,Miji na Majiji Ikulu Dsm
Moja ya jambo alilolisema limemsikitisha ni mitandao ya jamii kumuandika Luhende kama Msomi mwenye cheti cha hotel Management wakati ana Masters na alikuwa mkaguzi wa elimu wa kanda.

Rais anasema amepitia kwenye mtandao mmoja wa kijamii akaona comment za watu juu ya Luhende akabaki kucheka tu,amemsimamisha Luhende na kuwataka waandishi wa habari wampige picha na waende Sinza kumpiga picha Luhende Meneja wa Hotel nakuzisambaza mitanadaoni

Rais pia anasema anawafahamu Wakurugenzi wake wote,anasikia malalamiko kwenye mitandao ya kijamii,amewaambia wajishangilie wao na si kusikitika kwa kutokushangiliwa na mitandao ya kijamii,anasema hao wasioshangilia kwenye mitandao ni maadui zake,..."Watachonga sana lakini wataka kimya"

Rais anasema zamani nafasi za ukurugenzi zilikuwa "deal",na pale TAMISEMI kulikuwa na mtandao wa kuhongwa ili kuwapatia watu ukurugenzi,aliishagiza Waziri awaondoe wapo watatu pale utumishi ambao kazi yao ilikuwa kuhongwa na kugawa vyeo vya Ukurugenzi.Rais anasema Wakurugenzi wote aliwapitia jina kwa jina na ndio maana hasafiri ili kufanya mambo yeye mwenyewe na wakati mwingine hulala hata saa nane ili kujiridhisha mambo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top