Unknown Unknown Author
Title: AKILIMALI: SIJAMTUSI MWENYEKITI WANGU, MWENYEWE ASEMA NDIE ALIYEMUWEKA MADARAKANI NA KUVUNJA KATIBA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
AKILIMALI AFUNGUKA MUDA HUU TATIZO LAKE NA YUSUFU MANJI... " Sijamtusi mwenyekiti wangu kwa kusema amekurupuka . Neno hilo ni la k...
AKILIMALI AFUNGUKA MUDA HUU TATIZO LAKE NA YUSUFU MANJI...

" Sijamtusi mwenyekiti wangu kwa kusema amekurupuka . Neno hilo ni la kawaida wala sikuwa na dhamira ya kumtusi mwenyekiti wangu , nawaomba radhi wana yanga kwa kauli zangu . Usiku sijalala nilikosa raha mara baada ya kusikia Manji kajiuzulu".

Pia aliendelea kufunguka kwa kuzungumzia tatizo lao na Manji huku akisisitiza ushikamano kwa kusema "Mie naomba tuwe na umoja tatizo letu na mwenyekiti ni kushindwa kutuita wazee kwenye mpango wake wa kuichukua timu".

Huku akisisitiza kuwa wanampenda "Sisi tunampenda na kumuhitaji sana Yusufu lakini tunahitaji aendeleze mfumo wa zamani alioanza nao wa kujali na kuthamini wazee ili nasi tujisikie vizuri na klabu yetu", alisema.

"Nasisitiza sina chuki na Manji maana kwa mdomo wangu huu nimeshiriki sana kumuweka madarakani mpaka pale umma wa watanzania wakasema tumevunja katiba" alisema Mzee Akilimali.

Huku akimalizia kwa kusema "Ninachotaka alitambue baraza la wazee na sisi tukae nae tuzungumze mstakabali wa klabu yetu"
Mzee Akilimali Yahya.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top