Baada ya taarifa kwamba Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amejiuzulu uenyekiti kuzagaa, SALEHJEMBE ilifanya kila juhudi kumpata na mwenye akazungumza kwa ufupi.
Alipoulizwa kuhusiana na suala la kujiuzulu na pia kusitiza uamuzi wake wa kutaka kuwekeza au kuikodisha Yanga kwa miaka kumi, alisema basi imetosha.
“Kwa kweli imetosha, imetosha sasa,” alisema.
Alipoulizwa afafanue kuhusiana na kauli hiyo, Manji aliongeza.
“Nimesema hivi, imetosha. Naomba uniache, nisingependa kujibu lolote kwa sasa, niache tafadhari."
Kumekuwa na taarifa kwamba Manji ameamua kuachana na wazo lake la kuwekeza Yanga kwa miaka 10 baada ya kuona hata baadhi ya viongozi wa serikali wakimuandama kwa madai wanatumiwa na baadhi ya mamilionea.
Taarifa nyingine zimeelezwa kwamba, wako wanachama wa Yanga ambao wanaona hawatafaidika na maslahi yao binafsi kama Manji atawekeza, hivyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha haingii mkataba na kupewa nafasi hiyo kwa kuwa inaweza kuwavuruga.
Awali, kumekuwa na taarifa Manji ameamua kujitoa kwa kuwa kuna juhudi za chini pia zinazohusisha hadi watu wengine wenye mamlaka katika soka ambao wana hofu na uwekezaji wake.
Post a Comment